Home Audio JAPAN YAITUPA NJE ENGLAD NA KUTINGA FAINALI KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE

JAPAN YAITUPA NJE ENGLAD NA KUTINGA FAINALI KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE

SHARE
England women 1Timu
ya taifa ya wanawake ya England imetupwa nje ya michuano ya kombe la
dunia la wanawake kwenye mchezo wa nusu fainali kwa kichapo cha goli 2-1
kutoka  kwa Japan ambao ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo kwenye


michuano inayoendelea huko nchini Canada.

England womenJapani
walikuwa wakwanza kupata goli la kwanza dakika ya 33 kupitia kwa
 nahodha wao Aya Miyama baada ya Claire Rafferty kumfanyia madhambi
Saori Ariyoshi nje kidogo ya eneo la hatari lakini mwamuzi akaamuru
ipigwe penati na Miyami akaukwamisha mpira kambani.
England women 2Dakika saba baadae, England walisawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati pia kupitia kwa Fara Williams aliyefunga penati hiyo.
Goli la kujifunga la Laura
Bassett dakika za majeruhi liliwapa ushindi Japan na kuwapeleka kwenye
hatua ya fainali ambako watakutana na timu ya taifa ya Marekani.

SHARE