Home Audio Burundi, milio mengi ya masasi na ma bomu inazidi kuripotiwa pande zote...

Burundi, milio mengi ya masasi na ma bomu inazidi kuripotiwa pande zote za Bujumbura ata mikoani

SHARE
Hali
ya vuta ni kuvute inaendelea kote nchini Burundi ambapo mapambano makubwa
imeripotiwa sehemu mbalimbali. Milio mengi ya risasi na maripuko ya ma bom  imesikika katika tarafa ya Jabe, bwiza,
Ngagara, Cibitoke, Nyakabiga, Musaga na hata mkoani
Bujumbura vijijini. Baada ya
mashambulizi makali uko mkoani Kayanza na Muyinga, duru ya kuaminiwa zimetaja
kuwa kuna kundi kubwa ya watu wenye silaha nzito nzito walijaribu kuingia
nchini Burundi kupitia Gatumba na katika pori la Rukoko wakitokea nchini Congo.
Wakati hayo yakiendelea raisi Nkurunziza anaendelea na kampeni zake za kuania
kiti cha uraisi mkoani Bujumbura vijijini. Mpaka sasa jeshi wala polisi la
taifa awajakanusha wala kuthibitisha habarii hizi za mashambuzi makali sehemu
kadha nchini Burundi, jambo ambalo bila shaka inaendelea kukuza hofu na
wasiwasi mkubwa miongoni mwa raia. Hiyo jana tarehe 10 Julai mtu moja ndiye
amearithiwa kuuawa tarafani Buterere na mwingine kujeruliwa vibaya na askari
polisi walikua wakifyatuwa risasi ovyo. Kunako mapambano ya iyo jana Julai 10
jeshi la taifa na makundi la watu wanao bebelea silaha uko mkoani Kayanza tarafani
kabarore, tumepata habari kwa tukio ilo kwamba wajeshi wawili ndio
wameuawa  na wengine wengi kujeruliwana. Upande
wa jeshi wametaja kwamba wavamizi wawili ndio wameuawa na umoja kukamtwa. Nivigumu
wakati huu kujuwa ukweli na idadi rasmi ya vifu na majeruwi. Mwingoni mwa
vamizi aliye kamatwa alikua jeshi wazamani wa taifa ya Burundi, jambo ambalo
inathibitisha kwamba kuna wajeshi walio toroka kambi zao na kujiunga na
wapinzani wa Nkurunziza. Cha kushangaza hata watangazaji nasi waandishi wa
habari wanazuwiliwa kuingia kwenye hospitali kuliko ifadhiwa mihili ya majeshi
hao. Mashambulizi makali imeendeshwa katika kilima cha Buyumbu na wavamizi hao
wamethibitisha kuwa malengo yao ilikua kufika mjini kati Bujumbura ndipo
waanzishe mapambano makali. Tuwafaamishe kuwa hali hii mbaya ya Burundi imeanza
pale ambapo raisi Nkurunziza alipo tangaza dhamira yake yakugombea muula wa
tatu wakuongoza uliyo kinyume na katiba ya nchi na vile vile mkataba wa amani
wa Arusha. Hadi sasa watu zaidi ya 80 wamekwisha uawa na laki na nusu kuihama
Burundi na wa miya wametekwa nyara na idara ya Ujasusi ama documentation na
mpaka sasa aijulikani walipo na uku vijana mwengine wakishikiliwa rumande na
polisi kwa kosa pekee ya kushiriki kunako maandamano iliyo dumu kwa zaidi ya
miezi miwili. Kwa habari ambao tumeipata kwasasa kuna vijana wa 5 wameshikiliwa
uko mkoani Bubanza kwa kujaribu tu kuihama nchi ya Burundi kwa kuofia machafuko.

SHARE