Home Audio HII NI BARUA ALIYOANDIKIWA SHILOLE KUFUNGIWA KUFANYA KAZI ZA SANAA KWA MUDA...

HII NI BARUA ALIYOANDIKIWA SHILOLE KUFUNGIWA KUFANYA KAZI ZA SANAA KWA MUDA WA MWAKA MMOJA

SHARE
https://i2.wp.com/i.ytimg.com/vi/eMup7g-uOUM/maxresdefault.jpg?resize=640%2C344

Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) kama msimamizi na mratibu wa sekta ya Sanaa
nchini limemfungia msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Zuena Mohamed kwa
jina la kisanii Shilole kufanya shughuli za sanaa nchini kwa muda wa
mwaka mmoja kuanzia tarehe 24/07/2015 hadi tarehe 24/07/2016.
Itakumbukwa kuwa mnamo tarehe 09/05/2015 akiwa katika onyesho lake la
Muziki nchini Ubelgiji alikiuka maadili ya kazi ya sanaa mbele ya
hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania na hivyo akadhalilisha utu wake na
jamii ya Kitanzania kimaadili. Pia itakumbukwa kwamba mnamo mwezi
Oktoba, 2013 BASATA ilimuonya na akakiri kwa kuomba msamaha kwa tabia
yake ya kucheza bila kuzingatia utu na maadili awapo jukwaani.
BASATA ilimpa nafasi ya kutoa maelezo yake kwa nini asichukuliwe
hatua za kinidhamu kwa kitendo chake cha kudhalilisha maadili, utu na
sanaa ya Tanzania lakini akakaidi kutoa maelezo. Hivyo basi BASATA
imejiridhisha kwamba alikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onesho
lake la huko Ubelgiji makusudi na amekiuka Sheria, Kanuni na Taratibu za
uendeshaji wa Sanaa.
Hivyo basi kutokana na ukiukwaji huo wa sheria na kanuni za
uendeshaji wa shughuli za sanaa nchini, Baraza la Sanaa la Taifa chini
ya Kanuni ya 30(1)(d) ya G.N 322 ya 2005 limemsimamisha kujishughulisha
na kazi za Sanaa nchini kwa muda wa Mwaka Mmoja tokea tarehe 24/07/2015.
Hivyo haruhusiwi kufanya au kushiriki kwa namna yoyote ile shughuli
yoyote ya onesho la sanaa nchini au nje ya nchi. Iwapo atafanya kinyume
cha hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi ikiwa ni pamoja na yeyote yule
utakaye shirikiana naye.
Ni matumaini ya Baraza la Sanaa la Taifa kwamba wasanii na waandaaji
wa shughuli za sanaa wataendelea kutambua umuhimu wa kufuata sheria,
kanuni na taratibu zilizowekwa.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI