Home Audio HAKUNA KUCHELEWA, MESSI KUANZA MAZOEZI CHAMAZI LEO HUU NDIO MSHAHARA WAKE

HAKUNA KUCHELEWA, MESSI KUANZA MAZOEZI CHAMAZI LEO HUU NDIO MSHAHARA WAKE

SHARE
11737180_920557287983039_2068690925_n
Stori kubwa leo hii  ni
aliyekuwa winga wa Simba SC, Ramadhan Singano ‘Messi’ kusaini mkataba wa
miaka miwili katika klabu ya Azam fc, ikiwa ni siku mbili tu tangu TFF
wavunje mkataba wake na Wekundu wa Msimbazi.
Messi amesaini mkataba mnono kwa dau la milioni 50 na atakuwa analipwa mshahara wa Milioni 2 kwa mwezi.
Kabla ya kuingia katika mgogoro
wa kimkataba na Simba, Wekundu wa Msimbazi walitaka winga huyo asaini
mkataba wa miaka miwili kwa dau la milioni 30 na mshahara wa milioni
1.5, lakini alikataa.
SHARE