Home Audio Chile ndio mabingwa wa Copa America

Chile ndio mabingwa wa Copa America

SHARE

Chile imewashinda Argentina kupitia kwa mikwaju ya penalti na kushinda
kombe kubwa zaidi kati ya nchi za Marekani ya kusini la Copa Amerika.

nullSanchez

Hili ndilo kombe la kwanza la kimataifa kuwahi kushindwa na Chile.
Chile ambayo ni waandalizi waliwashinda Argentina mabao 4-1 kupitia mikwaju ya penalti baada ya timu zote kukosa kufunga.

nullWachezaji wa Argentina

Ni miaka 22 tangu Argentina washinde kombe lolote kubwa kwenye mashindano ya kandanda ya kimataifa.

nullMashabiki

Mchezaji wa Arsenal Alexis
Sanchez alifunga bao la ushindi baada ya mshambuliaji wa Argentina
Gonzalo Higuain kupiga nje huku mkwaju wa Ever Banega ukinyakwa na kipa
Claudio Bravo.

null Vidal

Awali Higuain alikuwa amekosa bao la wazi aliposalia na kipa baada ya dakika 90 za mchezo.

nullMessi kwa mara nyingine ashindwa kuipatia taifa lake taji

Sanchez karibia afunge katika dakika za ziada.

nullHiguain akikosa penalti

Miongoni mwa maelfu ya
mashabiki waliojaa kuishabikia timu yao ni wachimba mgodi 33 waliokwama
chini ya mgodi kwa wiki kadhaa mwaka 2010,katika kisa kilichovutia hisia
nyingi dunia

SHARE