Home Audio CHADEMA MOSHI MJINI WAMPITISHA JAFARY MICHAEL KUWANIA UBUNGE WA JIMBO HILO

CHADEMA MOSHI MJINI WAMPITISHA JAFARY MICHAEL KUWANIA UBUNGE WA JIMBO HILO

SHARE
Wajumbe
wa mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya
ya Moshi mjini wakiwa katika mkutano maalumu wa kumchagua mtia nia
atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu nafasi ya
Ubunge jimbo la Moshi mjini.
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge anayemaliza muda wake,Philemoni Ndesamburoakizungumza wakati wa mkutano huo.
Katibu
wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi mjini,Joel
Makwaia akizungumza katika mkutano wa Chadema alipoalikwa kukiwakilisha
chama chake.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
Katibu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya Moshi mjini,Leonard
Buberwa akizungungumza akati wa mkutano wa kumpata mgombea wa nafasi ya
Ubunge katika jimbo la Moshi mjini.
Watia
nia katika nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi mjini,Basil Lema,(kushoto)
Jafary Michael (katikati) na wakili wa kujitegemea ,Elikunda Kipoko
 wakiwa ukumbini kabla ya zoezi la uchaguzi kuanza.
Mbunge wa iti maalumu,Chadema,Lucy Owenya alikuwa ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Ubunge aliyejitokeza kutetea kiti chake.
Wajumbe wa mkutano wakishangilia mara baada ya kutangazwa kwa matokeo.
Msimaizi
wa Uchaguzi ,katibu wa baraza la wanawake mkoa wa Kilimanjaro ,Helga
Mchomvu akitangaza matokeo katika uchaguzi huo ambao mgombea Basil Lema
aliamua kujitoa kabla ya kura kupigwa.
Mtia nia aliyetangazwa mshindi Jafary Michael akiwa na mkewe katika ukumbi wa Umoja Hotel ambako uchaguzi huo ulifanyika.
Mmoja
wa wagombea wa nafasi hiyo aliyepata kura 9 ,Elikunda Kipoko
akizungumza na kuwashukuru wajumbe kwa wale waliompigia kura .
Jafary
Michael aliye chaguliwa na Chadema kupeperusha Bendera ya chama hicho
katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba katika kuwania kiti cha Ubunge
jimbo la Moshi mjini.
Michael aliyekuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,akimtambulisha mkewe mbele ya wapiga kura.
Mgombea
wa nafasi ya viti maalumu ,Lucy Owenya akiwashukuru wajumbe wa mkutano
huo kwa kumuamini na kumchagua tena kupeperusha bendera ya chama hicho
kupitia viti maalum.
Katibu
wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Basil Lema aliyekuwa miongoni mwa
wagombea kabla ya kujitoa akizungumza katika mkutano huo mara baada ya
Jafary Michael mkutano huo kupitisha jina lake kuwa mpeperushaji wa
bendera ya chama hicho katika jimbo la Moshi mjini.  
SHARE