Home Audio Nimezaa na Mose Iyobo lakini ndoa yangu ipo pale pale – Aunty...

Nimezaa na Mose Iyobo lakini ndoa yangu ipo pale pale – Aunty Ezekiel

SHARE

Muigizaji wa filamu, Aunty Ezekiel ambaye hivi karibuni alijifungua
mtoto wa kike, amedai kuwa licha ya kuzaa nje ya ndoa, bado anaamini
ndoa yake ipo pale pale.Akizungumza na Bongo5 leo, Aunty aka Mama Cookie, amesema aliamua kuzaa
na Moses Iyobo, dancer wa Diamond Platnumz kwakuwa muda wa kuwa mama
ulikuwa umefika.

Mimi niliamua kupata mtoto baada ya kuona wakati umefika,” amesema.

Kwasababu siku zinaenda pamoja na umri inabidi maisha yaendelee
mbele. Ndoa yangu ipo kama ilivyokuwa mwanzo, haijavunjika, sijawahi
kuongea kama nimezaa nje ya ndoa au ndani ya ndoa lakini mwisho wa siku
ndoa yangu bado ipo
,” ameongeza.

Haya ni maisha na vitu vinavyozungumzwa vipo kama vilivyo, lakini
familia yangu na watu wa karibu wanaelewa nini kinaendelea ndani yake na
watu niliokuwa nao wanaelewa na sidhani kama itakuwa right kuongea
kwenye media. Lakini watu wajue baba yake ni Mose
,” amesisitiza muigizaji huyo.

Pia Aunty amewatoa hofu mashabiki wa kazi zake kwa kusema kuzaa kwake sio mwisho wa kuigiza.

Kupata mtoto kwenye maisha yangu ni kitu kizuri kwa sababu kuna vitu
vingi ambavyo nimepunguza na nimekuwa mama mwenye majukumu, ninapofanya
vitu vyangu najua kesho na kesho kutwa kuna mtu ananitegemea. Pia kuzaa
kwangu sioo kwamba kutaua sanaa yangu, sanaa yangu ipo pale pale na
hata nitakapomaliza kulea nitakuwa na vitu vingi zaidi kwa sababu
natumia muda mwingi kulea Kwahiyo nikirudi wategemee vitu vikubwa zaidi
ingawa kuna kazi ambazo niliziandaa zitatoka wakati ninalea.

SHARE